Maandag, April 09, 2018

Njombe Mji FC yazidi kupunguza ubora wake.

Kivumbi cha Ligi Kuu Bara kiliendelea tena jioni ya jana kwa viwanja vinne kuwaka moto.

Padri auawa DRC


Vikosi vya Umoja wa Mataifa vikilinda amani DRCHaki miliki ya pichaAFP
Image captionVikosi vya Umoja wa Mataifa vikilinda amani DRC

Kasisi wa kanisa katoliki amepigwa risasi na kufa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo.
Vyanzo vya habari kutoka Kaskazini mwa jimbo la Kivu vimearifu kuwa Padri Étienne Nsengiunva alikuwa akikomnisha waumini na ndipo wakati mtu mwenye silaha alipoingia kanisani na kumpiga risasi.
Tukio hilo lilijiri wakati wa sherehe za ibada ya ubatizo wa wakristo wapya na wanandoa wapya.
Taarifa zinadai kuwa muuaji huyo ni kutoka katika kundi la waasi wa Mai Mai Nyatura ambalo ni miongoni mwa vikundi vinavyopambana kudhibiti jimbo hilo lenye rasilimali za madini lakini pia uporaji wa fedha kutoka kwa wanavijiji.

mubashara blog +255753121916

Waziri Mkuu awapa majukumu Mabalozi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchini Urusi na Rwanda kutumia fursa hiyo kwa kutangaza vivutio vilivyopo nchini ili kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii.

Adhabu ya Kifo Mali, yashutumiwa

Kikundi cha kutetea haki za binaadamu nchini Mali kimeshusha mzigo wa lawama kwa jeshi la nchi hiyo kutokana na kitendo cha kutekeleza adhabu ya kifo kwa wafungwa kumi na wanne katikati mwa jiji la Dioura.

Musiba awavaa TEF, awataka kutotumika kisiasa

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CZI Limited, Cyprian Musiba amelitaka Jukwaa la Wahariri kujitathmini na kujitafakari kuhusiana na matamko mbalimbali wanayoyatoa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 9



Sondag, April 08, 2018

watu 90 wauawa Douma, Syria kwa shambulio linalodhaniwa kuwa ya kemikali

Picha kwenye mtandao wa kijamii, inayodaiwa kuwaonyesha watoto wakitibiwa, kutokana na madhara ya shambulio hiloHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPicha kwenye mtandao wa kijamii, inayodaiwa kuwaonyesha watoto wakitibiwa, kutokana na madhara ya shambulio hilo
nukuu kutoka bbc swahili.
Rais wa Marekani Donald Trump amemkemea vikali rais wa Syria Bashar al-Assadna washirika wake Urusi na Iran juu ya shambulio linalodhaniwa kuwa ni la kikemikali, akisema kuwa kuwa "watakuwa na gharama kubwa ya kulipia shambulio hilo ".

Zaidi ya Wananchi 100 hawana makazi Msitu wa Tembo Simanjiro


Zaidi ya Wananchi 100 wa kijiji cha Msitu wa Tembo Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuanguka na kusombwa na mafuriko ikiwemo ya mwenyekiti wa kijiji hicho kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali .

Fuatilia Hapa Tukio la Kusimikwa Kwa Askofu Mkuu Jimbo Katoliki Arusha....Rais Magufuli Keshawasili

Misa na sherehe ya kumsimika aliyekuwa Askofu wa Jimbo la moshi Askofu Mkuu Mteule, Isaac Amani inaendelea katika Parokia ya Mt Mt. Theresia Arusha.

Mwakyembe anena neno zito.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, amewaasa Watanzania kuhakikisha wanapambana na viashiria vyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani na mauaji ya kimbari. Kauli hiyo  Dkt. Mwakyembe ameitoa wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu za mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda miaka 24 iliyopita.

BREAKING: MWANDISHI WA HABARI AVAMIWA NA WASIO JULIKANA

 Mmoja wa wahariri waandamizi wa gazeti la The Guardian, Finnigan Simbeye ameokotwa eneo la Bunju wilayani Kinondoni akiwa hajitambui.

Mwakyembe anena neno zito.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, amewaasa Watanzania kuhakikisha wanapambana na viashiria vyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani na mauaji ya kimbari. Kauli hiyo  Dkt. Mwakyembe ameitoa wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu za mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda miaka 24 iliyopita.

Meya aliyesifiwa na Rais asema kuhusu kuhama


Meya, Wajiji la Arusha, Kalista Lazaro (CHADEMA) amefunguka na kusema kitendo cha Rais kumsifia mbele ya hadhara ni heshima kwake na viongozi wa Arusha na kusema hakuna sababu kiongozi aliyechaguliwa na wananchi kuhama chama kwa kumuunga mkono Rais.