Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ameiagiza Idara ya Uhamiaji kuanza msako wa kuwakamata wahamiaji haramu waliojificha kwenye mashamba na majumbani.
Wanachama
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Monduli wameandamana kwenye
ofisi za chama hicho wakitaka aliyekuwa Mbunge wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo(CHADEMA), Julius Kalanga aliyejiunga na chama hicho kufuata
utaratibu ikiwemo hatua za uteuzi wa nafasi ya kugombania ubunge.
WAZIRI wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba amewataka waandaaji wa maonyesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane kuhakikisha kuanzia mwaka 2019 wanayaandaa katika sura mpya itakayoleta mabadiliko chanya kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili waweze kuzalisha kwa tija.
MBAO 75 na mitego miwili iliyokuwa inatumiwa na majangiri kutegea wanyama pori,kitongoji cha Namapwiya,Kijiji cha Mnyangala, Kata na karafa ya Mipingo,wilaya na mkoa wa Lindi,
Walimu wa Skuli binafsi wametakiwa kuhakikisha wanafuata Masharti na miongozo iliyowekwa na serikali ili kuimarisha Elimu ya msingi na sekondari na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametaka teknolojia mpya ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi inayooneshwa kipindi cha Maonesho ya maadhimisho ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama Nanenane iwafikie wananchi ili kuwakwamua katika dimbwi la Umasikini.
Madiwani wawili wa Chadema na NCCR-Mageuzi manispaa ya Bukoba wamejiuzulu uanachama na kujiunga na CCM, Akiwemo meya wa zamani wa manispaa hiyo, Dk Anatory Aman.
Watu wawili wamefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi cha udongo wakati wakichimba madini ya dhahabu katika machimbo madogo yaliyoko mtaa wa Buguti Kata ya Turwa wilayani Tarime.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla leo Jumamosi Agosti 4, 2018 amepata ajali eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini. Katika ajali hiyo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba amefariki dunia.