Saterdag, Augustus 04, 2018

MSANII WA HIP HOP "YLEEZ " KUTOKA NJOMBE AJA KWA MUONEKANO MPYA.



Msanii wa muziki wa Bongo Freva alimaalufu kama Hip Hop ajulikanaye kwa jina  YLEEZ amekutana na chombo chetu cha habari na kuzungumzia haswa
kazi yake muziki huo lakini pia amesema kwamba hivi kalibuni anatarajia kuachia wimbo Mpya utakao kwenda kwa jina la USIKONDE. 

Kazungumza hayo na mwandishi wetu Chrispin Kalinga alimaalufu kwa Jina la KIBOKO CHA MADANGA leo katika msako kwa msako ya Mubashara blog hapo mkoani njombe.

Sambamba na hayo Yleez aliongeza kwa kusema kuwa wimbo huo anao tarajia kuuachia siku ya kuzaliwa kwake ambayo ni August 13.Mwaka huu.
Hata hivyo msanii huyo amesema kuwa anawaomba mashabiki wake kuvuta subira kwa lengo la kuhakikisha ubora wa kazi hiyo ili kuufikisha mbali mziki wake.
   


Hapa katika picha {kushoto}ni presenter chrispin kalinga na{ kulia} katika Yleez ambaye mndiye msanii wa muziki huo.



Na hapa ni sehemu tu ya ofisi za Mubashara blog ambapo alifanikiwa kuingia ndani ya ofisi hizo akiwa yeye na mtangazaji.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking