Maandag, Augustus 06, 2018

Walimu watakiwa kufuata masharti na miongozo iliyowekwa na Serikali


Na. Thabit Madai, Zanzibar.

Walimu wa Skuli binafsi wametakiwa kuhakikisha wanafuata Masharti na miongozo iliyowekwa na serikali  ili kuimarisha  Elimu ya msingi na sekondari na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini.

Hayo yameibainishwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe,Riziki Pembe Juma wakati wa kuwakabidhi zawadi wanafunzi waliofaulu kidato cha sita   katika Shule ya sekondari ya Alhisani iliyopo  Mwanakwerekwe mjini Zanzibar.

Mhe, riziki alisema Kuna baadhi ya skuli nchini huwa hawafuati masharti na miongozo iliweka na serikali na kupelekea ufaulu mbaya na kuongeza ongezeko la wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo kuwa wengi.

Amesema skili hiyo mwaka huu imejitahidi kutoa wanafunzi thalathini na moja kwa ajili ya kujiunga na elimu ya juu hivyo lazima skuli zate  za binfsi  wazingatie  sheria na kanuni walizopangiwa na serilali ili kuondosha matatizo yanayojitokeza katika utendaji wa kazi  kwakufuata  mitaala  nakuhakikisha wanafundisha kwa kuchukua  juhudi  na sio kufanya biashara .

Aidha amewapongeza walimu na wanafunzi kujitahidi sana ili ufaulu wa wanafunzi kuweza kusoma kwa kuwelewa hasa masomo ya sayansi kwanini kumekuwa na upungufu wa wataalamu wa sayansi.

mkurungenzi wa direct aid sheikh  ayman  muhammed  kamaldin  amesema katika mwaka huu wanafunzi wa skuli hiyo wanatarajia kufanya vizur   kwa walivyojitayarisha na kuahidi kusaidia katika mambo ya uongozi wa skuli hiyo.

Mwalimu kuu wa skuli hiyo   Abdalah Nasosr amsema katika skuli hiyo wanaomba kupatiwa udhamini wa mikopo kwa wanafunzi ili waze kujiunga naelimu ya juu  na kushukuru wazazi na walimu kwa kuhakikisha skuli hiyo inarudisha heshima kubwa nakuweza kuto wanafuzi wengi ingawa hawakuwezakuto daraja la kwanza lakini daraja la pili ni wengi.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking