Maandag, Augustus 06, 2018

Mbao na mitego ya wanyama pori vya kamatwa Lindi


Na.Ahmad Mmow,Lindi.

MBAO 75  na mitego miwili  iliyokuwa inatumiwa na majangiri kutegea wanyama pori,kitongoji cha Namapwiya,Kijiji cha Mnyangala, Kata na karafa ya Mipingo,wilaya na mkoa wa Lindi,zimekamatwa baada ya kubainika zilivunwa kinyume cha sheria.

Hayo yameelezwa na ofisa ardhi na nal maliasili wa halmashauri ya  wilaya ya Lindi,Victor Shau,alipozungumza  na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ofisini kwake katika manispaa ya Lindi.

Zhao alieleza hayo baada ya kuombabufafanuzi juu ya kauli iliyokuwa imetolewa na mwenyekiti wa taasisi ya marafiki Waandishi wa Habari za Mazingira, Uoto wa asili na wanyamapori,Riziki Rulida,aliyoitoa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Lindi vijijini,wakati wa utambulisho wa Mradi wa Mazingira.

Shau akitolea ufafanuzi,amemtaja mfanyabiashara husika wa mazao hayo ya Misitu kuwa ni, Abdallah H.Wambili (bila ya kutaja anakoishi) huku aina ya Mbao zikitajwa kuwa ni Miti aina ya Mninga pamoja na Mvule.

Alisema mbao hizo zilikamatwa katija kitongoji cha Namapwiya, Kijiji cha Mnyangara,Kata na Tarafa ya Mipingo,wilaya ya Lindi,Julai 15 mwaka huu,saa 8:00 mchana,zikipakiwa kwenye lori ambalo hata hivyo hakuweza kutaja aina wala namba zake,tayari kupelekwa sokoni kwa mauzo.

Shau alisema licha ya mbao pia walikamata mitego miwili ya chuma ambayo ilikuwa ikitumiwa na majangili kutegea na kunasa wanyamapori.Wakiwamo tembo,nyati,kongoni,nyumbu,swala,simba,chui  na wengine wengi waishio porini Hata hivyo ofisa huyo hakuwa tayari kuweka bayana thamani ya mbao zilizokamatwa siku hiyo.

Shau alisema baada ya mahojiano na mfanyabiashara husika,leseni anayoimiliki inamruhusu kuvuna mazao hayo ya misitu ndani ya eneo la Kijiji cha Milola ‘B’ tarafa ya Milola.Hatahivyo Wambili,akitambua anachokifanya kuwa  ni kosa aliamua kuvuna katika Kitongoji cha Namapwiya, kijiji cha Mnyangara, Kata na Tarafa ya Mipingo.

Alisema mbao na gari  lililohusika kubeba mbao hizo,lipo chini ya uwangalizi wa serikali ya kitongoji cha Namapwiya,wakati taratibu zingine za kisheria zikiandaliwa.Zikiwemo ya kumtoza faini kwa kosa linalomkabili,ambayo kwa fedha za kitanzania ni kati ya shilingi 500,000/-hadi  2,000,000.

Awali akiutambulisha mradi wa uhifadhi mazingira kwa madiwani hao,mwenyekiti wa taasisi ya marafiki waandishi wa habari za mazingira,uoto wa asili na wanyamapori,Riziki Rulida ameliuomba uongozi wa halmashauri  hiyo ya Lindi,kuliangalia eneo la Tendeguru kwa jicho la huruma kufuatia uharibifu unaofanywa na binaadamu.

Rulida alisema kutokana na hali aliyoiona eneo hilo,ambalo ni maarufu kwasababu ndipo alipotoka mjusi aitwae Dynasoo,akunakila sababu ya kukomesha hali hiyo.Kwani kama jambo hilo lisipofanyika kwa haraka kunauwezekano mkubwa eneo hilo kugeuka jwangwa.

‘’katika msafara wetu tumeweza kukamata mbao 75 na mitego ya miwili ya chuma iliyokuwa inatumiwa na majangili kuwanasa wanyama’’ Alisema Rulida.

Mkoa wa Lindi nimiongoni mwa maeneo makubwa yenye misitu.Huku ukipakana na hifidhi Selous,ambayo ni kubwa ikilinganishwa na mbuga nyingi zilizo ndani na nje ya nchi.Hata kunachangamoto ya uwindaji haramu na uvunaji misitu ovyo.


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking