Saterdag, Augustus 11, 2018

YLEEZ " KUTOKA NJOMBE AACHIA WIMBO WAKE ''USIKONDE''


Msanii wa muziki wa Bongo Freva  Hip Hop ajulikanaye kwa jina  YLEEZ  Kutoka Mkoani Njombe amekutana na Mubashara blog na kuzungumzia kazi yake ambayo anaichai siku ya leo inayo kwenda kwa jina la  USIKONDE.
Wakati huo pia Msanii huyo amesema kuwa siku mbili zijazo itakuwa ndiyo siku ya kuzaliwa kwake sambamba na hayo ameweka wazi kuwa wimbo huo utapatikana katita mitandao ya kijamii. 

YLEEZ akaongeza kwa kusema kuwa mara nyingi anatambua uwepo wa vyombo vya habari kuwa vinaumuhimu gani katika kuendeleza mziki wake Nukuu " natambua umuhimu wa vyombo vya habari kama redio lakini pia blog vyombo hivi vya habari vimefanyika msaada mkubwa kwangu kwa kunitambulisha kwa watanzania wengi ambao walikuwa hawanijui lakini sasa wananiofahamu ndio maana naviheshimu sana vyombo vya habari pamoja na watu wake ambao ni waandishi wa habari na watangazaji"Amesema. Kayaongea hayo leo na mubashara blog.

 
mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking