Sondag, Augustus 26, 2018

Mbosso afichua uhusiano wa wimbo wake na kuachwa kwa Diamond na Zari


Msanii wa muziki Bongo, Mbosso amesema si kweli kwamba wimbo wake unaokwenda kwa jina la Nimekuzoea alimuimbia Diamond Platnumz baada ya kuachwa na mzazi mwenzie, Zari The Bosslady.

Muimbaji huyo kutokea WCB katika mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema wimbo huo ulikutana na tukio hilo na ulikuwepo kwa kipindi kirefu.

"Hapana, ni wimbo ambao ulikutana tu na tukio, ni wimbo wangu ambao nilishawahi kuimba zamani sana kipindi nipo Yamoto Band," amesema.

"Sasa nilipokuja kuingia WCB ni moja ya nyimbo zangu alikuwa anazipenda sana Bosi (Diamond), akaniambia inabidi uufanye, sasa kipindi ambacho nautoa ndio ua mwana  wa weusi," amesema Mbosso.

Wimbo wa Mbosso, Nimekuzoea ulitoka February 09, 2018 wakati usiku wa February 14, 2018 ambayo ilikuwa ni siku ya Wapendanao (Valentine Day) ndipo Zari The Bosslady aliposti Ua Jeusi kwenye ukurasa wake wa Instagram na kueleza kuwa ameachana rasmi na Diamond Platnumz.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking