Sondag, Augustus 26, 2018

Muro afanya ziara ya kushtukiza, abaini raia tisa wa kigeni wasio na vibali


Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amefanya ziara ya kushtukiza  katika barabara ya mchepuko Arusha Bypass katika eneo la muungano Makumira  na kubaini uwepo wa vitendo vinavyoashiria ukiukwaji wa taratibu za kazi na haswa katika kazi zinazofanywa na raia kutoka nje.

Muro Pamoja na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo itakayosaidaia kupunguza msongamao wa magari kuelekea Jiji la Arusha ameonyeshwa kukerwa na tabia ya baadhi ya wageni kufanya kazi zinazoweza kufanywa na watanzania jambo linalominya fursa ya vijana wa kitanzania kupata ajira.

Kutoka na sababu hiyo Dc Muro alilazimika kuchukua hatua  ya kuwaagiza maofisa wa Uhamiaji kufuatilia suala hilo jambo lililopelekea kubainika uwepo wa raia tisa ( 9 ) wa kigeni wanaofanya kazi hizo pasipo kuwepo na baadhi ya vibali husika vya kufanya kazi.

Katika ziara hiyo Dc Muro aliambatana na Naibu katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote ambao ni waratibu wa ujenzi wa Barabara hiyo.

Dc muro anaendelea na zoezi la ukaguzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi katikaa wilaya ya Arumeru yenye kata 53 na Halmashauri mbili za Arusha Dc na Meru Dc


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking