Matukio ya Madiwani kuhama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) yamezidi kushika kasi, baada ya diwani wa tano wa Kata ya Olsunyai, Elirehema Nnko, kuhama chama hicho jana.
Aidha, tangu kuanza kwa matukio ya kujiuzulu madiwani wa chama hicho mwaka jana, hadi sasa wamefika watano walioachia ngazi.
Madiwani wa Chadema waliojiuzulu na na kjiunga CCM ni Credo Kifukwe (Muriet), Geyson Ngowi (Komandolu), ambao tayari kaza zao uchaguzi umesharudiwa na CCM kuzinyakua.
Wengine ambao wamejiuzulu karibuni na uchaguzi bado kufanyika ni Elirehema Nnko (Olsunyai), Prosper Msofe (Daraja Mbili) na Obeid Meng'oriki wa Kata ya Terati.
Akizungumza jana wakati akitangaza kuachia ngazi Chadema na kujiunga CCM, Elirehema alisema sababu kubwa ya kuhama ni za kibiashara.
“Biashara zangu haziendi vizuri nadhani nikiwa CCM zitabadilika natakuwa nzuri,”alisema.
Sababu hiyo aliyotoa diwani huyo inakuwa tofauti na walizotoa wenzake waliomtangulia kutoka chama hicho ambao wanadai sababu kubwa ni kuguswa na jitihada za Rais John Magufuli na kuamua kumuunga mkono kwa kujiunga na chama tawala.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking