LUDEWANA MAIKO LUOGA LUDEWA
Waumini wa Kikiristo wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe wametakiwa kuwa na moyo wa Upendo ikiwa ni pamoja na Kujitolea katika Kujenga Nyumba za Ibada katika maeneo yao ili siku ya Mwisho Mwenyezi mungu aweze Kuwabariki.
Wito huo umetolewa January 15 mwaka huu 2018 na Wachungaji wa Kanisa Anglican Mtaa wa Ibumi na Amani Ambao ni Mchungaji Dismas Mgina Wa Amani na Mchungaji Lameck Luoga wa Ibumi wakati wakiuaga Mwili wa Aliyekuwa Fundi Mkuu katika Ujenzi wa Jengo la Kanisa Anglican Mtaa wa Ibumi Marehemu John Haule Aliyezaliwa Mwaka 1981 na Kufariki Mwaka huu 2018.
Katika Hatua Nyingine Wachungaji hao waliiasa Jamii ya Ludewa na Mkoa wa Njombe kwaujumla Kuitunza na Kuisaidia Familia aliyoiacha Marehemu John Mke na Mtoto Mmoja Pekee wakike Mona Haule anayesoma Kidato cha Pili katika Shule ya Sekondari Luana kwani Msaada mkubwa Ulikuwa kwa baba yake mzazi ambae Ameiaga Dunia hivyo Mtoto huyo Anahitaji msaada wa Wadau ili aweze kuendelea na Masomo yake.
Baadhi ya Wananchi wa kata ya Ibumi Na wengine kutoka Nje ya Ibumi waliojitokeza katika Mazishi ya Fundi huyo wa Ujenzi na Mdau wa Mpira wa Miguu wamemzungumzia Marehemu John Enzi za Uhai wake Akiishi na jamii kabla ya Kukutwa na Mauti hapo Janury 14 Mwaka huu 2018 Baada ya Kuugua Muda mrefu Homa ya Mapafu Kujaa maji na Moyo kupanuka wakisema kuwa Marehemu John Alikuwa na Umoja na ushirikiano kwa Jamii pia alikuwa Mjumbe wa kamati ya Shule ya Msingi Ibumi Enzi za Uhai wake.
Ilikutoa msaada wako kwa Familia ya Marehemu john Ili mtoto wake aendelee na Masomo wasiliana na Mwandishi wa Habari Hizi kupitia Simu namba +255762705839 Ili kumwezesha Binti huyo kuendelea na Masomo, Kutoa ni Moyo Si Utajiri.
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe Amen,
Chrispiny kalinga blog
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking