Dinsdag, Maart 06, 2018

Manispaa ya Kinondoni Kuboresha Mambo saba

Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo wamefanya mkutano wa Baraza la Madiwani ambapo wamepitia makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida wa mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019.

Akiongoza kikao hicho meya Benjamini sita amesema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatarajia kukusanya kiasi cha Tshs 242,186,292,987.00 ambapo Tshs 686,380,000.00 sawa na  0.3 no mchango wa Jamii na Tshs. 32,062,704,908,00 sawa na 13.2% ni Mapatoya ndani ya Manispaa

Aidha katika Fedha hizo Halmashuri ya hiyo inatarajia kukusanya kiasi cha Tshs 32,749,084,908.00 kutoka vyanzo vyake vya ndani amabapo Tshs 16,392,166,400.00 zitatumika Kwa matumizi ya kawaida na Tshs 16,356,913,913,508.00 zinatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Fedha na ruzuku kutoka Serikali kuu, ni Tshs 209,436,208,079.00 zitakazojumuisha kiasi cha Tshs 103,934,539,473.00 Kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Tshs 105,501,668,606.00 kwa ajili ya miradi ya maedendeleo

Hata hivyo kutokana na bajeti maeneo yaliyopewa kipaumbele katika mpango huu ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Manispaa, kuboresha miundombinu ya kiafya, shule za msingi na Sekondari, kuboresha miondombinu ya maji, Barabara, kilimo, miradi ya maendeleo, ukusanyaji taka, na kuboresha mazingira ya wafanya biashara wadogowadogo

Kupitia kikao hicho wajumbe ambao ni madiwani walipitisha bajeti hiyo ya mwaka 2018/2019 ambapo halmshauri ya Manispaa hiyo imeahidi kuweka  mahusiano mazuri na Serikali pia mashirika  yasiyo  kiserikali.


Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking