WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya ya Bagamoyo wametakiwa kutembea kifua mbele huku wakijiamini na kuwaelezea vijana wenzao miradi mbalimbali mikubwa inayofanyika hapa nchini chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais,Dk.John Magufuli katika kutimiza malengo ya Tanzania ya Viwanda kwa kujenga barabara za juu (Fly Over),uboreshaji wa miundombinu,mradi wa umeme vijijini (REA),elimu bure shule za msingi na sekondari,ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kisasa ya Standard Gauge,ununuzi wa ndege za Bombadier pamoja na kutumbua watumishi vyeti feki.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Makwiro wakati akizungumza na vijana wa UVCCM wilayani Bagamoyo jana kwenye muendelezo wa ziara yake ya kutembelea wilaya zote za mkoa wa Pwani ambapo amewashukuru na kuwakumbusha vijana hao kuishi katika ndoto ya Rais Dk.John Magufuli na malengo ya kuifanya nchi kuwa Tanzania ya Viwanda katika hotuba waliyozungumza katika mkutano mkuu wa vijana hao uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni ambapo katika mkutano huo ulimwezesha Kheri James kuwa mwenyekiti wa UVCCM Taifa.
“Nimekuja katika Wilaya hii ya Bagamoyo kwa ajili ya kutoa shukrani zangu kwa ninyi vijana wenzangu kwa kuniamini na kunipigia kura za ndiyo zilizoniwezesha kushinda nafasi hii ya uenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani hivyo basi nitatumia akili zangu,nguvu,uwezo,rasilimali na elimu niliyonayo katika kuhakikisha natatua changamoto za vijana wa mkoa wetu wa Pwani leo kichama naonekana nawawakilisha vijana wa Chama Cha Mapinduzi peke yake lakini ukweli ni kwamba nitakachokipigania mimi kitawaletea faida vijana wote wa mkoa huu hivyo kwa yale nitakayokuwa nayapambania kwa vijana nanyi muwe bega kwa bega mniunge mkono katika kufanikisha changamoto za vijana” Alisema Mwenyekiti Makwiro..
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking