Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefunguka na kuzungumzia suala la maandamano na kusema atashughulika na watu ambao wataandamana ili wakawasilimulie wale watu ambao wamewatuma.
Rais Magufuli amesema hayo leo Machi 9, 2018 wakati akizindua tawi la benki ya CRDB Chato na kusema kuwa wapo watu ambao wanataka kuona amani ya nchi hii inavurugika jambo ambalo yeye hawezi kukubali kwa kuwa alihapa kulinda Katiba ya nchi.
"Wapo watu wameshindwa kufanya siasa za kweli wangependa kila siku tuwe barabarani tunaandamana, watu wao wanahamia huku wao wanataka wabaki wanaandamana kule
"Nimeshasema ngoja waandamane wataniona, kama kuna baba zao wanawatuma basi watakwenda kuwasilimulia vizuri, niliapa kwa Katiba kwamba nchi hii lazima iwe ya amani na tunataka tujenge uchumi wa kweli ili Watanzania watajirike na hali ya Watanzania imeanza kwenda vizuri
"Mwanzo ni mgumu lakini nataka niwaambie watanzania tupo kwenye wakati mzuri tuvumiliane ili tufike sehemu Tanzania iwe nchi ya asali" alisema Magufuli.
Chrispiny kalinga blog
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking