Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam imemhukumu msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohamed maarufu Shilole kulipa faini ya kiasi cha shilingi milioni 14, baada ya kupatikana na hatia ya kutapeli na kusababisha hasara kwa kushindwa kufika kwenye tamasha.
Katika kesi hiyo imethibitika kuwa Shilole alilipwa kiasi cha shilingi Milioni tatu na Mary Musa ambaye ndiye muandaaji wa shoo hiyo, ili aweze kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka wa mwaka jana, 2017 katika ukumbi wa Heineken uliopo Mbagala-Kijichi jijini Dar es Salaam, lakini hakufika kama walivokuwa wamekubaliana.
Baada ya mashabiki waliokuwa wameahidiwa kupata burudani kutoka kwa Shilole kutokumuona, walipandwa na hasira na kufanya vurugu kubwa iliyosababisha uharibifu wa mali za thamani ya shilingi milioni 14.
Kutokana na kitendo hicho, Mahakama imemuamuru Shilole kulipa kiasi hicho cha fedha kama fidia kwa mlalamikaji ambaye ni Mary Musa.
Chrispiny kalinga blog
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking