BAVICHA Wamshambulia Kwa Maneno Katibu Mkuu BAVICHA Baada ya Kudai Tundu Lissu ni Muongo na Anatafuta Umaarufu
January 11, 2018
Katibu
Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA)
Julius Mwita amefunguka na kusema kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka huenda ana
matatizo ya akili.
Mwita amesema hayo leo Januari 11, 2018 katika Mkutano na waandishi wa habari wakati akijibu tuhuma alizotoa kiongozi huyo wa UVCCM dhidi ya Tundu Lissu ambapo alisema kuwa Tundu Lissu ni muongo na hapaswi kuaminiwa kwani atafuta tu umaarufu.
Kufuatia
kauli hiyo ya Shaka ndipo hapo viongozi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA
walipoaamua kujitokeza na kuzungumzia juu ya kauli hizo za kijana wa CCM
na kusema kuwa;
"Tumetafakari kauli ya Shaka kwa kina na tumejaribu kufikiri kama Shaka ana akili timamu au ni kichaa? Kwa sababu kama chama chake chenyewe wamekiri pamoja na Serikali hawawezi kuzungumza suala la Lissu kwa sababu ni mgonjwa na yupo hospitali, Shaka anapata wapi ujasiri wa kuja kuzungumza mambo yanayomuhusu Tundu Lissu tena kwa kuzungumza mambo ya uongo na ushahidi usio na tija yoyote na anawadanganya Watanzania kuwa katika nchi hii Lissu siyo wa kwanza kupigwa risasi" alisema Mwita

Aidha
kiongozi huyo wa BAVICHA amemtaka Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana
Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka alisimame na kusema mpaka
sasa Tundu Lissu ametibiwa kwa fedha ya Serikali shilingi ngapi.
"Tulitegemea
umoja wa vijana wa chama ambacho kinaendesha Serikali watoke wawaambie
Watanzania kwamba tunakitaka chama chetu yaani kiiagize Serikali kutibu
mgonjwa ambaye yupo hospitali na ameshambuliwa katika majukumu yake ya
Ubunge lakini Shaka anatoka kupotosha kwa maneno ya kejeli na ya
kihuni.
"Lakini tumkumbushe Shaka, Amani Abed Karume hakuuawa kwa sababu za kisiasa na wala hajawahi kuwa mpinzani, wala hajawahi kuwa mkosoaji wa Serikali iliyopo madarakani kwa wakati huo useme kwamba alishambuliwa kwa sababu ya ukosoaji wake bali kulikuwa na sababu zingine tofauti zilizopelekea Karume kushambuliwa"

Siku
kadhaa zilizopita Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alifunguka na
kuishtumu Serikali ya awamu ya tano kuhusika katika kushambuliwa kwake
baada ya kali hiyo Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka naye amlijibu Tundu Lissu na kusema
kuwa mwanasiasa huyo ni muongo na anatafuta umaarufu.
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking