Donderdag, Januarie 11, 2018

LUDEWA

NA Mwamwa Kalinga Chrispin


Baada ya Wanafunzi wa Darasa la Awali na Darasa La kwanza Kuripoti kwa wingi Kuanzia Jumatatu ya January 08 Shule ya Msingi Kimbila iliyopo Ludewa Mjini Katika Mkoa Wa Njombe imebainika kuna inaupungufu mkubwa wa Vyumba vya madarasa pamoja na Ukosefu wa Jiko la kupikia Chakula cha wanafunzi shuleni hapo.

Wakizungumza na Kituo hiki Baadhi ya Walimu pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shule ambao walikutwa wakipokea michango ya chakula, Maji pamoja na Ulinzi kutoka kwa Wazazi Waliopeleka watoto wao shuleni hapo wamesema Kuwa Wanafunzi wanaofika kusoma katika Shule hiyo ni Wengi lakini Shule inakabiliwa na Uhaba mkubwa wa Vyumba vya madarasa.

Hatahivyo Uongozi wa Shule ya Msingi Kimbila Umeituhumu Serikali ya Kijiji cha Ludewa Mjini kuwa Haipo Tayari Kusimamia Shughuli za Maendeleo katika Shule hiyo hasa katika Ukarabati wa Majengo yaliyochakaa pamoja na Ujenzi wa Jiko la Kuandalia Chakula cha Wanafunzi.


KIBOKO CHA MADANGA Ameshuhudia Zoezi la Usajiri wa wanafunzi wa Darasa la Awali na Darasa la kwanza kwa mwaka huu 2018 Likiendelea Huku wazazi wakiendelea kutoa michango wanayotakiwa Kuitoa hasa Mwanzoni mwa mwaka huu 2018 kisha Wazazi wa wanafunzi wakazungumzia Zoezi hilo.

Katika Hatua nyingine Kituo hiki kimemtafuta Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Ludewa Mjini Bw, Omari Kiowi ili Kuzungumza juu ya Ushiriki wa Serikali yake katika Ujenzi wa Shule hiyo ambaye anakiri Kuzitambua changamoto zinazoikabili Shule hiyo ikiwemo Ukosefu wa Jiko la Chakula Shuleni Hapo.

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking