Sondag, Februarie 04, 2018

MWENYEKITI CCM ATIA FOLA,,,,.

 
 Na Maiko Luoga Ludewa. 
Maadhimisho ya Sherehe za miaka 41 Tangu kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM kwa wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Maadhimisho hayo yanafanyika Leo
katika Kata ya Mlangali Ambapo Wananchi wa Wilaya ya Ludewa wametumia nafasi hiyo kumtumia salamu za Pongezi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kwakazi Kubwa anayofanya ya Kurejesha Nidhamu na Uchumi wa nchi.

Wakizungumza na Mtandao huu wa www.maikoluoga.blogspot.com wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali waliokusanyika kusherekea Maadhimisho hayo yanayofanyika Mlangali wamesema kuwa Wanampongeza Rais Magufuli kwakushughulikia Matatizo ya Utumishi na mishahara Hewa, Wanafunzi hewa Pamoja na Kuwashughulikia Watendaji wa Serikali wasio waaminifu katika Serikali yao iliyowapa Madaraka. 
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ya Miaka 41 Tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM Ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Njombe Bw,Erasto Ngole maarufu kwa jina la Shikamoo Parachichi ambae anajumuika na Wanachama, Wapenzi na Wakeleketwa wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Ludewa chama ambacho awali kilijulikana zaidi kwa jina la TANU na katika Mkutano huo Baadhi ya waliokuwa wanachama wa vyama vingine vya siasa wilaya ya Ludewa wanatarajia kujiunga na Chama cha mapinduzi. 
Asante Endelea kuwa nasi Tutakuletea Habari Kamili ya Maadhimisho hayo ya miaka 41 ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ludewa kwasasa Mkutano unaendelea katika Viwanja vya Ofisi za CCM Itundu kata ya Mlangali Wilayani Ludewa.Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking