Woensdag, Februarie 28, 2018

Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havijawekwa kwa nia ya kulididimiza taifa

Korea Kusini inadai kwamba vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Korea Kaskazini havikuwekwa kwa nia ya kulididimiza taifa hilo bali kulisaidia.

Hayo yamezungumwa na waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini  Kang Kyung-wha wakati wa mkutano kuhusu silaha wa Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano huhuo Korea Kaskazini nayo haijakubaliana na suala hilo na kutahadharisha kuwa huenda vikwazo hivyo vikaharibu mahusiano mazuri kati ya Korea Kusini na Kaskazini.

Korea Kusini imesema inaamini vikwazo hivyo vimewekwa kwa nia ya kuikumbusha Korea Kaskazini kuwa maisha yake ya baadae hayategemei silaha za nyuklia bali yanategemea ushirikiano wa taifa hilo na uliwengu katika kupunguza utumiaji wa silaha.

Hata hivyo balozi wa Korea Kaskazini Han Tae Song ameishutumu Marekani na vikwazo vyake na kusema kuwa hatua hiyo haitoitisha Korea Kaskazini wala kubadilisha lolote.

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking