Woensdag, Februarie 28, 2018

Linah aweka wazi aina ya mwanaume anayemtamani kuwa nae

Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga maarufu kama 'Ndege Mnana' amekuwa miongoni mwa wanawake wachache wanaovutiwa kimahaba na wanaume wenye rangi ya ngozi nyeusi tofauti na wengine wanavyochagua watu wa kuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi.

Linah amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii facebook wa EATV kila Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

"Mimi napenda wanaume weusi, warefu si unajua mimi mfupi (shoti), sipendi wanaume weupe japo nishawahi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume mweupe ambae ni Naga aliyekuwa ananisimamia katika kazi zangu hata ile ya 'project' yangu ya Ole Temba", amesema Linah.

Pamoja na hayo, Linah ameendelea kwa kusema "rangi yangu si kwamba najichubua hapana, saizi watu tunaoga vizuri, sina 'stress' zozote, naweza kununua mafuta mazuri ya kupaka tofauti na enzi zile tunapaka mafuta ya mgando".

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking