Woensdag, Februarie 28, 2018

Trump amtaja Parscale kama meneja wa kampeni zake za 2020

Rais wa Marekani Donald Trump amemtaja meneja wa kampeni zake za urais mwaka 2020.

Brad Parscale mtaalam wa mitandao, alifanya kazi katika kampeni za Trump 2016 na alisifiwa sana kwa kutumia mitandao ya kijamii vizuri jambo linalotajwa kumpa ushindi Trump.

Parscale atatumika katika kampeni za uchaguzi mdogo baadae mwaka huu, Trump anasema Parscale ni mtu sahihi na amekuwa akifanya kila kitu kwa uhakika wa hali ya juu.

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking