Woensdag, Februarie 21, 2018


Mkuu Wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere Akifafanua Lengo halisi la Mkutano huo,
Na Maiko Luoga Ludewa. 
Mkuu Wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Mh, Andrea Tsere Amewataka Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari Ambao Shule zao Zimeshika Nafasi za Mikia zilizopo Katika Makundi ya Shule Kumi Duni Kwa matokeo ya Darasa la Saba na kidato cha Nne mwaka 2017 Wajiudhuru Nafasi zao za Ukuu wa Shule kwakuwa Wameshindwa Kutekeleza Majukumu yao.

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Ametoa Maagizo hayo Jana Jumanne February 20/2018 Kwenye Mkutano wa Wadau wa Maendeleo Wilaya ya Ludewa Mkutano Uliofanyika Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ukiwa na Lengo Kubwa la Kujadili Kiwango cha Elimu Katika Wilaya ya Ludewa ambapo Shule za Msingi na Sekondari za Wilaya ya Ludewa kwa miaka Mitano iliyopita Zimekuwa zikifanya Vibaya Katika Matokeo yake na Kushika Nafasi za Mwisho Kimkoa.

Wakihojiwa Na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa kwanini Shule zao zimefanya vibaya katika matokeo ya Darasa la Saba na Kidato cha Nne mwaka 2017 Walimu wakuu ambao Shule zao zimefanya vibaya Walimweleza Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Kuwa Uhaba wa Walimu, Kufanyiwa Vitendo vya Ushirikina kwa Walimu na wanafunzi katika Baadhi ya Shule pamoja na Mazingira Magumu ya Kufanyia Kazi Ni Changamoto Kubwa Zilizosababisha Shule zao Kufanya Vibaya. 

Kwaupande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Mundindi Mwalimu John Mtweve Alimweleza Mkuu wa Wilaya ya Ludewa kuwa Shule yake imefanya Vibaya kwakuwa yeye alikuwa na Kazi nyingine za kusimamia maendeleo ya Shule hiyo hali iliyomlazimu Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere Kumwagiza Afisa Elimu Sekondari Bw. matenusi Ndumbaro Kutengua Nafasi ya Mkuu huyo wa Shule na Kumpangia Mkuu mwingine kusimamia Shule ya sekondari Mundindi.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Amemwagiza Afisa Elimu wa Shule za Msingi Bw, Christopher Wangwe Kumshusha Cheo Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Lihagule Kutokana na sababu ya Shule yake kufanya vibaya na kushindwa Kufika katika kikao kilichoitwa na Mkuu wa Wilaya Bila kutoa sababu yeyote iliyomfanya Ashindwe Kuhudhuria Mkutano huo wa Kujadili Kiwango cha Elimu Wilaya ya Ludewa.

Baadhi ya wajumbe waliopata nafasi ya Kutoa maoni yao ya kuboresha Elimu katika Wilaya ya Ludewa Akiwemo Bw, Johson Mgimba ambae licha ya kuahidi Kuchangia Mafuta ya Gari Lita 300 Kwaajili ya Kuboresha Safari za Ukaguzi kwa Shule za Msingi pia aliibua Hoja ya kuanzisha mfuko wa Elimu ili wadau wachangie mfuko huo kisha Hoja hiyo ikaungwa Mkono kikamilifu na Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh, Deo Ngalawa Pamoja na wajumbe wote wa mkutano Kisha Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Akatoa wito Kwa wadau Kujiandaa Kuchangia Mfuko huo Baada ya Utaratibu kukamilika. 

Kuhusu Mikakati na Nini kifanyike Ili kukuza kiwango cha Elimu Katika wilaya ya Ludewa Wadau wameshauri Kuwa Uandaliwe Mfuko Maalumu wa Elimu ili Wadau wa Elimu waweze kuchangia kupitia mfuko huo, Ni lazima kuwepo na Makambi kwa madarasa ya mitihani Katika muda wa likizo na Wazazi pamoja na wadau wachangie Uendeshaji wa Makambi hayo. 

Wadau hao pia Wakiwemo Maofisa kutoka katika Shirika la SHIPO Wameongeza kuwa Wanafunzi wa Elimu za Juu muda wa likizo Warudi Ludewa Kuwasaidia Wadogo zao, Kwakuwa Elimu ni Gharama Wazazi ni lazima wachangie Chakula ili wanafunzi wale chakula Shuleni, Walimu wakuu wa Shule ni lazima Wawajibike Katika nafasi zao, na Mkutano Huo utakuwa unafanyika kila Mwaka mwanzoni na Mwisho wa mwaka.

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking