Sondag, Februarie 11, 2018

MAHANDI YAUZWA KAMA MTUMBA

Picha ya Ado Junior
Wafanya biashara wilayani njombe mkoani njombe wialalamikia Serikali kwa kufunga mipaka ya kutoa mahindi yasitoke nje ya Nchi kwa madai nchi iwe na chakula cha kutosha 

Wafanya biashara hao wameendelea kwa kulalamika kuwa mahindi hayo wakiya jumua kwa wakulima wana baki nayo katika maghara yao kwa sababu wateja wanao taka mahindi ni watu wadogowadogo wanao nunua mahindi kwa ajili ya kula wao wenyewe na familia zao kwahiyo yanabaki yamejazana kwenye maghala na kupata hasara nyingine ya kuharibika kwa mahindi hayo.
Katika hatua nyingine wameeleza kuwa hapo awali mahindi yalikua hayajai kwenye maghara yao kwani yakifika tu yanapitiliza kwenda nchi nyingine ila sasa yanabaki tu kwenye ghala yanaharibika na mengine kuoza kabisa hali hii imekua ikiwakatisha tamaa wafanya biashara hao hadi kuperekea kuto kuipenda kazi yao.
Mbali na hivo wameiomba serikali kuwa saidia kivyovyote vile ili waweze kuwa kama awali kwani mpaka sasa hali bado no ngumu mahindi in mengi kwenye maghala Wateja hawapo na mahindi mengine yamekua yakihalibika hadi kuwaperekea kuuza kwa bei ya chini bado Wateja hawapo hivo kupata hasara kubwa sana kiuchumi "tunaomba serikali itusaidia kwa hili kwani mpaka sasa tunateseka sana"alisema moja kati ya wafanyabiashara mkoani njombe.

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking