Dinsdag, Maart 20, 2018

PADECO, WAFUNGUA MAISHA YA WANANCHI WA LUDEWA,NA MKOA WA NJOMBE

Katikati ni Mkurugenzi wa PADECO Bw,Wilbard Mwinuka Akiwa na Wafadhiri kutoka nchini Hispania

Mkurugenzi wa PADECO Wilbard Mwinuka akizungumza katika Ukaguzi wa Mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Chief Kidulile Ludewa Mjini,
DC, Ludewa Mh, Andrea Tsere akizungumza na wananchi wa Ludewa mjini waliojitokeza katika Ukaguzi wa Mabweni ya chief Kidulile
Mkurugenzi wa Ofisi ya maendeleo Jimbo Catholic la Njombe FR,Lugome akizungumza na wakazi wa Nindi juu ya Mradi wa maji kijiji cha Nindi na Ntumbati katika kata ya Lupingu
Wafadhiri wa Mradi wa Maji kijiji cha Maholong'wa Kupitia PADECO Wakizindua Rasmi Mradi huo
Hiki ni kituo cha maji katika Shule ya Msingi Maholong'wa katika Kata ya Ludende,
Mkurugenzi wa Shirika la PADECO Bw, Wilbard Mwinuka akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Maholong'wa wilayani Ludewa,

Na Maiko Luoga Ludewa.
Shirika la Participatory Development Concern (PADECO). Kwakushirikiana na Jimbo Catholic la Njombe kwa kipindi cha mwaka 2018/2019 wamekusudia Kukamilisha Miradi ya maji katika Vijiji vya Kitewele, Mavanga, Iwela, Nindi na Ntumbati Wilayani Ludewa katika Mkoa Wa Njombe Vijiji ambavyo vimekuwa na Changamoto ya maji kwa muda mrefu.

Akizungumza na Mtandao huu Mkurugenzi wa Shirika la PADECO Mkoa Wa Njombe Bw,Wilbard Mwinuka Amesema kuwa Licha ya Kupeleka maji katika vijiji hivyo pia Shirika kwa kushirikiana na Jimbo Catholic la Njombe wamefika nakuona Changamoto ya Ukosefu wa Huduma ya Afya na Maji katika Kijiji cha nindi nakuahidi Kutafuta namna ya Kuboresha Kituo cha Afya Nindi ambacho Majengo yake yamechakaa Kutokana na Ukongwe wake.

Aidha Shirika la PADECO na Jimbo Catholic la Njombe wamefanikisha Kupeleka Huduma ya Maji Wilayani Ludewa katika Vijiji vya Ugera, Muhumbi-Lipangara, Luvuyo Pamoja na Ujenzi wa Mabweni Mawili katika Shule ya Sekondari Chief Kidulile iliyopo Ludewa Mjini na Shirika hilo pamoja Na Jimbo Catholic la Njombe kwa umoja wao wameendelea kuzindua na kusimamia Miradi ya maji katika Vijiji vya Maholong'wa Kupitia Ludea, Luana Kupitia Mladea na Muholo Kupitia Yorda.
 
Mkurugenzi wa PADECO Bw, Wilbard Mwinuka akiambatana na Mkurugenzi wa Ofisi ya Maendeleo Jimbo Catholic Njombe Fr. Hermengird Lugome Wameongoza msafara wa wafadhiri ambao ni Wanawake Watatu Kutoka Shirika la MANOS UNIDAS lenye makao yake Makuu katika Mji wa Madrid Nchini Hispania Kutembelea na Kukagua Baadhi ya Miradi wilayani Ludewa ambayo imefadhiriwa na Shirika hilo kutoka Nchini Hispania.

Wafadhiri hao watatu Kutoka Nchini Hispania Ambao ni Jimena Franco's, Flori Langdon, pamoja na Livia Alvarez walitembelea na Kukagua Miradi Mbalimbali wilayani Ludewa ambayo wamekuwa wakiifadhiri kwa wananchi na kujionea Miradi hiyo ikiendelea Vizuri huku wakiahidi Kuendelea Kushirikiana na wananchi Wa Ludewa Kupitia Shirika La PADECO.

Kwaupande wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Kupitia Mwenyekiti Wa Halmashauri hiyo Mh, Edward Haule, Makamu Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mh, Monica Mchilo Pamoja na Wataalamu Mbalimbali wa Halmashauri Hiyo Akiwemo Muhandisi Wa Maji wilaya ya Ludewa Enjinia Nasibu Mlenge Wamewashukuru Wafadhiri Kwakusaidia Kutatua Shida za Wananchi wa Ludewa.

Baadhi ya Shughuli zilizofanywa na Wafadhiri Mbalimbali Wilayani Ludewa na Nje ya Ludewa Kupitia Shirika la Participatory Development Concern (PADECO) nipamoja na Ufadhiri Wa aina mbalimbali kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Ludewa, Vyuo vya Ufundi na Vyuo vikuu katika Mikoa Mbalimbali Hapa nchini Tanzania tangu mwaka 2012.
Kutoa vifaa vya maabara na Umeme katika zahanati ya Misheni Kijiji cha Luana, Kuwezesha Ufadhiri wa Mabweni Shule ya Sekondari Madunda na Shule maalumu Mundindi, Kufanya Uwezeshaji wa Shughuli za Upandaji miti, Kutunza Mazingira na Vyanzo vya Maji katika Mkoa wa Njombe.

Aidha Shirika la PADECO Limeweza kukabidhi mashine ya Utra Sound katika Hospital ya Wilaya ya Ludewa pamoja na Kufadhiri Ukarabati na Umaliziaji wa Mradi wa Shule ya Mpya ya Msingi Sambala iliyopo katika kata ya Mawengi Pia PADECO Wamefanikisha kukamilisha Kazi ya Uwekaji Umeme katika Shule ya Sekondari Luana iliyopo katika kata ya Luana wilayani Ludewa. 

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking