Dinsdag, Maart 20, 2018

MWALIMU AWAPELEKA WANAFUNZI KULIMA SHAMBA LAKE LUDEWA,



Na Maiko Luoga Ludewa

Wananchi Wa Kijiji cha Mdilidili katika Kata ya Lugarawa Wilaya ya Ludewa Mkoa Wa Njombe wamelalamikia Tukio la Mwalimu Wa Kujitolea Katika Shule ya msingi Matika iliyopo katika Kijiji cha Mdilidili Kuwachukua watoto Siku ya Jumamosi March 17 Mwaka huu na kuwapeleka Shambani kwake Kulima.


Waandishi Wa Habari wakiwa katika Safari za kikazi siku ya jumamosi Kutoka Kata ya Madilu kuelekea Ludewa Mjini walipofika Njiani katika Eneo la Kinyangesi Kijiji cha Mdilidili Kuelekea Mkongobaki walikutana na Msafara Wa wanafunzi waliovalia Nguo za kawaida wakiwa wamebeba Majembe na Baada ya Kuhojiwa wanafunzi hao walijitambulisha kuwa wametoka Shule ya Msingi Matika wanaelekea Shambani kwa Mwalimu wao.

Wakati mazungumzo na watoto hao yakiendelea Walitokea Wananchi Waliokuwa Wakielekea Shambani Ambao walizungumzia Tukio hilo na Kusema kuwa Watoto wao waliaga Nyumbani kuwa wanaenda kufanya Mtihani Shuleni Lakini Walishangazwa Kuwaona Watoto hao wakiwa na Majembe wanaelekea Kulima Shamba la Mwalimu wakujitolea Ambae analipwa Posho kila mwezi kutokana na Michango ya Wazazi.

Alipoulizwa Mwalimu huyo Wa kujitolea katika Shule ya Msingi Matika Aliyejitambulisha kwa Majina ya Ester Mgani Alisema kuwa Amekuwa Akijitolea kuwafundisha Watoto hao kwa Muda wa Ziada hivyo Baada ya kufanya Mtihani Aliwaomba watoto wamsaidie Kulima Shamba lake na Kisha Kuondoka nao Kuelekea Shambani bila kutoa Taarifa kwa Mwalimu wake Mkuu Wa Shule ya Msingi Matika Akiamini Yupo Sahihi kutokana na Makubaliano yake na Wanafunzi.

Kwaupande wake Mwalimu Mkuu Wa Shule ya Msingi Matika Mwalimu Upendo Mluwili Amesema kuwa Siku ya  Jumamosi yeye alikuwa kwenye Kikao Hivyo Hakuwa na Taarifa yoyote Kuwa wanafunzi wameelekea Shambani kwani aliamini kuwa wapo Darasani.

Aliongeza Kuwa Majira ya Saa sita Mchana siku hiyo ya Jumamosi Alifuatwa na Mwalimu Huyo aliyewapeleka watoto Shambani akimweleza tukio hilo kuwa ameonana na Waandishi Wa Habari njiani akiwa na Wanafunzi kuelekea Shambani kwake Ambapo Mwalimu huyo Mkuu amesema kuwa Mwalimu wake ametenda kosa Bila kujua kwakuwa Mwalimu huyo ni wakujitolea hajawahi Ajiriwa na Serikali.

Bw. Aliponda Shaula Ni Mwenyekiti Wa serikali ya Kijiji cha Mdilidili katika Kata ya Lugarawa Akizungumza na Mwandishi wetu kwa Njia ya Simu Amekiri Kupokea Taarifa hiyo na Kulaani kitendo kilichofanywa na Mwalimu huyo wa kujitolea kwakuwa yeye analipwa posho kwa mwezi kutokana na Michango ya Wazazi na kuongeza kuwa Mwalimu huyo alitakiwa kutoa Taarifa kwa uongozi Wa juu ili aweze kusaidiwa kabla ya kujiamria mwenyewe.


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking