Woensdag, Maart 14, 2018

Msanii wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka sababu ya baadhi ya mstaa hasa wa kike kutodumu katika mahusiano.
Image result for Shamsa Ford
Muigizaji huyo amesema mahusiano ya watu maarufu hayadumu kutokana wanaingiza umaarufu wao katika mahusiano yao. Kupitia ukurasa wake Instagram Shamsa ameandika;
“Nimegundua mahusiano mengi ya watu maarufu hayadumu kwa sababu wengine huwa wanaleta Ustar hadi kwenye mahusiano, hata mtu wa kawaida akiwa na uhusiano na mtu maarufu ni mara chache sana kudumu,” amesema.
“Hasa kwa upande wa wanawake huwa tunaamini ustar ndo kila kitu kwa mwanaume kumbe sio, sasa sijui hatuna elimu ya ustar au vipi kwa hapa Bongo, maana ingekuwa ustar shida Beyonce na Jay Z wasingedumu mpaka leo na hawa ndo mastar wa dunia,” amesisitiza.
September 2016 Shamsa Ford alifunga ndoa na mfanyabiashara wa maduka ya nguo Rashidi Saidi a.k.a Chidi Mapenzi

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking