Saterdag, Maart 10, 2018

MWENYEKITI WA CHADEMA AKIMBILIA CCM

Mwenyekiti Wa UV, CCM Mkoa wa Njombe Bw, Neemia Tweve Akimkabidhi Kadi Bw, Benai Mgaya aliyejiunga na CCM Leo Ludewa Mjini. 
Bw, Benai Mgaya Akila Kiapo cha uadilifu wa Chama mbele ya Viongozi na Wanachama wa UV, CCM Katika Ofisi za CCM leo. 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Liwigi Katika kijiji na Kata ya Mlangali wilayani Ludewa KatikaMkoawaNjombe Kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bw, Benai Mgaya Amejiudhuru nafasiyake na kujivua uanachama Wa Chadema na Kutangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.
Bw, Benai Mgaya Ametangaza Kujivua Uanachama wa Chadema na Kujiunga na CCM Mapema hii leo Katika Mkutano wa UV, CCM Uliofanyika Leo Katika Ofisi za CCM Ludewa Mjini mbele ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Njombe Bw, Neemia Tweve Ambapo Mwanachama huyo mpya wa CCM amesema kuwa Sababu ya Kuachana na chama chake cha Chadema ni kutokana na Kutoridhishwa na Mwenendo na Msimamo wa chama hicho kwasasa.

Akimkabidhi kadi ya Uanachama wa CCM Pamoja na kadi ya Umoja wa Vijana Mwenyekiti wa UV, CCM Mkoa wa Njombe Bw, Neemia Tweve Amemkaribisha Mwanachama huyo na Kumtaka Aendelee kuwa mwanachama wa Kudumu ndani ya Chama cha Mapinduzi.

Kwaupande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa Bw, Bakari Mfaume Amesema kuwa Katika Kipindi cha Mwaka huu 2018 Wenyeviti watatu wa vijiji na vitongoji waliokuwa Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wameachana na Chama hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi.

Katika ziara yake Wilayani Ludewa Mwenyekiti wa vijana wa CCM Mkoa wa Njombe Bw Neemia Tweve ameongozana na Katibu wa Vijana Mkoa wa Njombe Ndg, Sure Mwasanguti, Mjumbe wa Baraza Kuu UV, CCM Taifa Mkoa wa Njombe Ndg, Omega Thobias, Pamoja na Ndg,Ocol Haule Ambae ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UV, CCM mkoa wa Njombe. 

Baada ya Kuwasili Wilayani Ludewa Viongozi hao wa vijana wa CCM Mkoa wa Njombe Walipokelewa na Viongozi wa Umoja huo wa Vijana Wilaya ya Ludewa Akiwemo Mwenyekiti wa Umoja huo Bi, Theopister Mhagama Pamoja na Katibu wake Bw, Hassan Kapolo kisha wakakaribishwa kwapamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa Bw, Bakari Mfaume. 

Mwenyekiti wa UV, CCM Mkoa wa Njombe Bw, Neemia Tweve amesema kuwa Lengo la Ziara hiyo Katika Wilaya za Mkoa Wa Njombe ni Kuboresha Siasa Inayoendana na Uchumi kwa upande wa Vijana Ikiwa ni Pamoja na Kujiunga Katika vikundi mbalimbali vya Uchumi ili waweze Kujiinua Katika Maisha yao. 

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking