Saterdag, Maart 24, 2018

MWANAFUNZI APIGWA NA RADI AFARIKI LUDEWA,


Na Maiko Luoga Ludewa.

Tukio lililotokea siku  March 20 mwaka huu la Kupigwa na Radi Wanafunzi 26 Katika Shule ya Msingi Itundu iliyopo katika Kata ya Mlangali wilayani Ludewa katika Mkoa Wa Njombe Limesababisha Kifo cha Mwanafunzi Mmoja Aliyeitwa Sophia Msemwa aliyekuwa na Umri Wa Miaka 12 Mwanafunzi Wa Darasa la Sita.

Tukio hilo lilitokea siku hiyo  Majira ya Saa Saba Mchana wakati Wanafunzi Wakipata Chakula Cha Mchana Nje ya Majengo ya Shule na Kuwajeruhi wanafunzi hao 26 Ambapo Baada ya Kufikishwa Kituo cha Afya Mlangali Mwanafunzi Sophia Msemwa Alifariki Dunia Muda Mfupi Baadae Kutokana na Kujeruhiwa Vikali na Radi hiyo.

Evodia Mgimba ni Mwalimu Mkuu Wa Shule ya Msingi Itundu Amesema kuwa Radi hiyo pia Ilivunja Vioo katika Ofisi ya Walimu pamoja na Kuvunja Dirisha Eneo Ambalo Marehemu Aliketi akipata Chakula Cha Mchana katika Nyumba ya Mwalimu Mkuu ambayo kwasasa Haishi Mtu.

Kwaupande wake Diwani Wa Kata ya Mlangali Mh. Hamis Kayombo Ametoa wito kwa wananchi Wa Kata yake kuhakikisha Wanashirikiana ili waweze Kujenga Mabwalo kwaajili ya Chakula, Wazazi kuwaandalia watoto wao Sare Za Uhakika ikiwemo Viatu Pamoja na Kuiomba Serikali Kuweka Mitego ya Kuzuia Radi katika Taasisi Mbalimbali.

Wadau Mbalimbali kutoka Idara ya Elimu Wilaya ya Ludewa wameshiriki mazishi ya Mwanafunzi Huyo Sambamba na Kutoa Pole Kwa Wafiwa

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking