Donderdag, Maart 15, 2018

Rais Trump amteua mtangazaji wa televisheni kuwa mshauri mkuu wa Uchumi





Trump amteua Kudlow kuwa mshauri mkuu wa masuala ya uchumi .Mchambuzi wa masuala ya fedha katika televisheni nchini Marekani, Larry Kudlow sasa atakuwa mshauri mkuu mpya wa masuala ya uchumi katika Ikulu ya Marekani ya White house.
Kudlow amelieleza shirika la habari la AP kuwa amekubaliana na uteuzi huo wa rais Donald Trump kuhudumu kama mshauri wa masuala ya uchumi. Kudlow atachukua nafasi ya Gary Cohn ambaye alitangaza wiki iliyopita kuwa atajiuzulu nafasi hiyo baada ya kupinga mipango ya rais Donald Trump inayohusiana na viwango vipya vya kodi kibiashara. Kudlow mwenye umri wa miaka 70 ni mchambuzi mwandamizi katika kituo cha Televisheni cha CNBC.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking