Dinsdag, Maart 13, 2018

Theresa May: Urusi imehusika kumshambulia Sergei Skripal

May anasema matukio kama hayo yanaaribu taswira ya nchi
Image captionMay anasema matukio kama hayo yanaaribu taswira ya nchi
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amasema kuwa serikali yake ina amini kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa Urusi imehusika katika shambulio la mpelelezi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na mtoto wake wa kike, lilitokea kusini mwa Uingereza katika mji wa Salisbury.

Aidha Bi May ameongeza pia inawezekana tukio hilo limelengwa moja kwa moja na Urusi dhidi ya Uingereza ama Urusi imeshindwa kudhibiti kemikali zake hatari.
''kuna mambo mawili tu yanaweza kuhusika kwa shambulio lilotokea, inawezekana serikali ya Urusi ilikusudia kufanya tukio hili hapa Uingereza, ama imeshindwa kudhibiti silaha hizi hatari za kemikali na hivyo imesababisha imetumiwa na watu wengine'' Alisema May.
Sergei Skripal(kulia) na binti yake bado wapo mahututi hospitalini
Image captionSergei Skripal(kulia) na binti yake bado wapo mahututi hospitalini
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ameunga mkono Uingereza kwa kusema kuwa huenda Urusi inahusika moja kwa moja katika shambulio hilo, kwa upande wake msemaji wa ikulu ya white house Sarah Sanders ametoa pole na kwa raia wa Uingereza bila kuunga mkono shutuma ya Uingereza kwa Urusi.
kwa upande wake mbunge kutoka chama tawala nchini Urusi , Vitaly Milonov amesema kuwa shambulio hilo dhidi ya mpelelezi wa zamani ni mbinu iliyotumika kuihusisha Urusi na si vinginevyo.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking