Saterdag, Maart 24, 2018

ZAIDI YA WANACHAMA 320 WAJIUNGA NA UWT,CCM CHUNYA,MBEYA

Wanachama wapya wa CCM Wakila kiapo cha Uadilifu wa Chama mbele ya Mgeni Rasmi

 Na Maiko Luoga,
Zaidi ya Wanachama 320 Kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wamejiunga na Jumuiya ya UWT Pamoja na Chama cha mapinduzi CCM Leo na Kukabidhiwa Kadi za Chama hicho kisha Kula kiapo cha Uadilifu wa Chama cha Mapinduzi CCM.

Wanachama hao wapya wa UWT na CCM Wamejiunga na Chama hicho Mapema siku ya jana Katika ziara ya Naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM, UWT Tanzania Bara Bi, Evah Kihwele Mwingizi Aliye ambatana na  Katibu wa Idara ya Organization UWT Taifa Bi, Rizicki Kingwande Katika Halmashauri ya Chunya Mkoani Mbeya.

Wakiwa Katika ziara hiyo viongozi hao wa Kitaifa wamefanikiwa Kutembelea kituo cha Watoto yatima kinachomilikiwa na Kanisa la Morovian kilichopo katika eneo la Chunya Mjini, Pia wametembelea Nyumba ya muda mrefu ya UWT iliyozinduliwa na Bi, Sophia Kawawa Pamoja na Kuongoza Harambee ya pesa kwaajili ya Akina mama wawili ambao ni Walemavu kwaajili ya Kujikimu.

Aidha katika Ziara hiyo pia walishiriki Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chunya pamoja na Mkoa wa Mbeya Lengo likiwa ni kuzidi kuimaarisha Chama hicho pamoja na Jumuiya zake ili kuweza Kushughulika na Shida za watu wa Tanzania. 


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking