Dinsdag, Maart 20, 2018

MOTO ULIOUWA MAJENGO YA BWENI





Na Maiko Luoga Ludewa.

Bweni la Wanafunzi Wavulana wa Kidato Cha Tano na Cha Sita katika Shule ya Sekondari Chief Kidulile iliyopo katika Kata ya Ludewa Mjini wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe Limeteketea Kwa Moto Usiku wa Leo.

Bweni hilo lililokuwa likitumiwa na wavulana 83 Wa Kidato cha Tano na Sita Katika Shule ya Sekondari Chief Kidulile Limeteketea kwa Moto Usiku wa Leo March 19/2018 Kuanzia Majira ya saa Tatu Usiku Wakati wanafunzi wakiwa Darasani wakiendelea na Masomo ya Muda wa Usiku.

Kwamujibu wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Chief Kidulile Mwalimu Aloice Kapelela Chanzo cha Mlipuko wa Moto huo bado hakijafahamika maramoja Pia Hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa wala Kupoteza Maisha Wote wamebaki salama Vifaa ndio vilivyoungua Kwa Asilimia Kubwa.

Licha ya Jitihada za kuzima Moto huo zilizofanywa na wadau mbalimbali waliokusanyika katika eneo la tukio Hazikuweza kuzaa matunda kutokana na Kukosekana kwa Vifaa vyenye Ubora kwaajili ya Kuzimia moto huo Hali iliyosababisha Paa lote la jengo hilo kuteketea Kwa moto pamoja na Vifaa mbalimbali vya wanafunzi yakiwemo Masanduku waliyohifadhia Vifaa.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking