Dinsdag, Maart 13, 2018

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 13.03.2018

Aliyekuwa kocha wa Souampton Mauricio Pelegrini
Image captionAliyekuwa kocha wa Souampton Mauricio Pelegrini
Aliyekuwa mkufunzi wa Watford Marco Silva ni miongoni mwa wakufunzi wanaopigiwa upatu kuchukua kazi ya kuikochi Southampton kufuatia hatua ya klabu hiyo kumfuta kazi kazi kocha wake Mauricio Pellegrino siku ya Jumatatu.. (Mail)
Wakati huohuo, Silva anatarajiwa kurudi nyumbani kwao Portugal ambapo anakaribia kuafikia makubaliano ya kuwa kocha mpya wa Benfica. (Times - subscription required)
Image captionMshambuliaji wa Tottenham Harry Kane
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane amehusishwa na uhamisho wa Real Madrid lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amesema kuwa atasalia kuichezea Tottenham kwa kuwa anasubiri kufunga mabao zaidi katika uwanja mpya wa timu hiyo. (Telegraph)
Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho ameiambia Real Madrid kufikiria kuhusu mchezaji mwengine katika usakaji wa kipa kwa kuwa anaamini David de Gea, 27, atasalia katika klabu hiyo. (Express)
Image captionMatumaini ya Liverpool na Manchester United kumsajili beki wa Lazio Stefan de Vrij, 26, kulia huenda yakaendelea
Matumaini ya Liverpool na Manchester United kumsajili beki wa Lazio Stefan de Vrij, 26, huenda yakaendelea baada ya Inter Milan kushindwa kuthibitisha kwamba watakuwa wakimsajili beki wa Uholanzi ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu. (star)
Juventus ina wasiwasi huenda ikamkosa kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can, ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu huku Bayern Munich na Real Madrid zikiwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ujerumani. (Express)
Chelsea inamnyatia kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma, 19, iwapo kipa wa Ubelgiji Thibaut Courtois, 25, ataondoka Stamford Bridge. (Corriere dello Sport, via Talksport)
Image captionChelsea inamnyatia kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma, 19, iwapo kipa wa Ubelgiji Thibaut Courtois, 25
Newcastle itajaribu kumsajili winga wa Chelsea aliyepo katika klabu hiyo kwa mkopo kwa mkataba wa kudumu lakini italazimika kulipa hadi £15m kumnunua mchezaji huyo wa Brazil ,mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)
Newcastle, Leicester na Southampton wanamtaka winga wa Burnley mwenye umri wa miaka 27 Johann Berg Gudmundsson. (Sun)
Image captionBarcelona imekuwa ikimnyatia kwa miezi kadhaa sasa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 26,
Barcelona imekuwa ikimnyatia kwa miezi kadhaa sasa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 26, baada ya mchezaji huyo kutokubaliana na Atletico Madrid kuhusu kuongezewa kandarasi yake. (Le10sport.com - in French)
Mkufunzi wa West Brom Alan Pardew atasalia katika klabu hiyo licha ya kuwa na mpango wa kumsajili kocha mpya mwisho wa msimu huu (Mirror)
Image captionArsenal inamchunguza mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri baada ya kufurahishwa na hatua ya kuibandua Tottenham katika kombe la vilabu bingwa . (star)
Arsenal inamchunguza mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri baada ya kufurahishwa na hatua ya kuibandua Tottenham katika kombe la vilabu bingwa . (star)
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Paul Merson anaamini kwamba mkufunzi wa Celtic Brendan Rodgers anafaa kumrithi Arsene Wenger kuwa mkufunzi wa Gunners . (Sky Sports, via Express)
Image captionHector Bellerin kulia wa klabu ya Arsenal
Arsenal iko tayari kumuuza Hector Bellerin ili kusaidia kujijenga upya , lakini wanataka £50m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. Klabu ya Juventus imeonyesha hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa Uhispania.
Philippe Coutinho anasema kuwa angependelea mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 Neymar kurudi Barcelona . Neymar alijiunga na PSG kutoka Barca kwa dau lililovunja rekodi la £198m mwisho wa msimu uliopita kabla ya mchezaji mwenza wa Brazil Coutinho, 25, kuelekea Nou Camp kutoka Liverpool mnamo mwezi Januari. (Mail)
Image captionPhilippe Coutinho anasema kuwa angependelea mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 Neymar kurudi Barcelona
Mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri ameomba msamaha kwa matamshi ya ubaguzi wa kijinsia aliyotoa kwa mwanahabari mmoja wa kike baada ya mechi ya ligi ya seria A siku ya Jumapili.. (Mail)

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking