Saterdag, Februarie 03, 2018

Masoko ya mazao kuimarishwa



Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuimarisha masoko ya
mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kupata tija.

Taarifa iliyotolewa leo Februari 3, 2018  na ofisi ya Waziri Mkuu inaeleza kuwa ametoa kauli hiyo jana Januari 2, 2018 wakati akikagua Kampuni ya Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha masoko.

Amesema kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali imedhamiria kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.

“Kupitia Wizara ya Kilimo tunataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini. Wakati umefika kwa wakulima nchini kuona tija ya mazao wanayolima,” amesema.

Ametoa mfano zao la pamba ambalo wakulima walikuwa wanaingia mikataba na wanunuzi, mfumo ambao ulikuwa unawanyonya badala ya kuwanufaisha.

Awali, ofisa mtendaji mkuu wa TMX, Godfrey Malekano amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa wamejipanga vyema kuanza minada ya mazao.

“Tutaanzia na zao la ufuta mwezi Mei, 2018 na kuendelea na mazao mengine kwa kadiri ya misimu ya mazao hayo ilivyo,” amesema.

Amesema kufanikiwa kwa soko la bidhaa na mfumo wa stakabadhi ghalani kunategemea msaada wa Serikali, “Soko la bidhaa la Ethiopia linalotajwa sana kwa mafanikio limefikia malengo yake kutokana na mkono wa Serikali.”

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking