Saterdag, Februarie 03, 2018

Mrema awatolea uvivu UKAWA


Mwenyekiti wa chama cha TLP Lyatonga Augustino Mrema amefunguka na kusema kuwa UKAWA hawampendi wala hawamtaki ndiyo maaana walifanya kila
namna kuhakikisha wanampokonya jimbo la Vunjo kwa kumsimamisha James Mbatia katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Mrema amesema hayo jana Januari 2, 2018 akiwa kwenye kampeni za kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia chama cha TLP, Dokta Godfrey Malisa na kusema kuwa wapinzani nchi hii wamekuwa wakimchukia.

"Ni kweli kwamba UKAWA hawanipendi, hawanitaki wakaninyang'anya lile jimbo wakampa James Mbatia angekuwa basi anafanya kazi za wananchi wa Vunjo wala nisingelalamika. Angelikuwa mwaminifu kwa Rais wetu wala nisingehangaika wala kulalamika, lakini walininyang'anya jimbo kwa ulaghai na utapeli kwa maneno ili kunimaliza kwa wananchi wa Vunjo wakasema Mrema ni mzee na kweli ni mzee ila kuwa mzee siyo kosa wala siyo dhambi kwamba wazee hawana manufaa" alisema Mrema

Mbali na hilo Mrema aliendelea kusema

"Hawa UKAWA wananiita marehemu mtarajiwa ndiyo wenzangu kwa hiyo wakaninyanyasa, wakanizodoa na ndiyo maana nawaambia UKAWA wakiendelea na tabia hii ya kuwakataa wazee kama Mrema kama hawana lolote, hamtakaa mpate kura za wazee wa nchi hii kwa sababu maneno yenu waliyasikia. Kwanini mnatukataa sisi wazee"


Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking