Vrydag, Februarie 02, 2018

Rais Magufuli Amtumbua Mwanasheria Mkuu wa Serikali....



Rais Magufuli amefanya uteuzi mpya kwa kumteua Dk Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais Magufuli pia amewateua aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Naibu wake, Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu, kuanzia leo.

Kabla ya uteuzi, Dk Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (St.Augustine University) kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta, (Tanzania Petroleum Upstream Regulatory Authority- PURA).

Taarifa ya Ikulu imeeleza pia kuwa, Naibu Mwanasheria Mkuu Paul Ngwembe kabla ya uteuzi, alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tanzania Insurance Regulatory Authority-TIRA).

Wateule wote wanatarajiwa kuapishwa Jumamosi asubuhi tarehe 3 Februari 2018.

Awali katika maadhimisho ya Siku ya Sheria, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli katika hotuba yake, aliwanyooshea vidole Waziri wa Katiba na Sheria, Prof Palamagamba Kabudi, na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Naibu wake Gerson Mdemu wameshindwa kuandaa kanuni za msaada wa kisheria.

Rais Magufuli alitoa mwezi mmoja kwa viongozi hao, kukamilisha kanuni za msaada wa kisheria, huku akiongeza kuwa  usimamizi wa sheria na utoaji wa haki, bado una changamoto, kwani wapo wachache, uadilifu wao na matendo yao yanachafua vyombo nyeti.



Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking