Vrydag, Februarie 02, 2018

SHEREHE ZA MIAKA 41 YA CCM KUFANYIKA MLANGALI, LUDEWA,

NJOMBE-MLANGALI

Na chrispiny kalinga


PICHA NA...MAIKO LUOGA

Katikati ni Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bw, Bakari Mfaume Kulia ni Bw, Leodgar Mpambalyoto Katibu wa siasa na Uenezi Wilaya ya Ludewa na Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Mlangali
 Wakiwa Katika
kikao na Wajumbe

Baadhi ya viongozi wa CCM Tarafa ya Mlangali wakiwa Katika Kikao cha maandalizi ya sherehe za miaka 41 ya CCM Katika Ukumbi wa CCM Mlangali

Katika Kusherekea Miaka 41 tangu kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM Hapa Nchini Tanzania Uongozi wa chama hicho Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe ukiongozwa na Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa bw, Bakari Mfaume Leo wamefanya kikao cha mwisho Katika Ukumbi wa ofisi ya CCM Mlangali Tayari kwa sherehe hizo zitakazo fanyika Kiwilaya Katika kata ya Mlangali Siku ya jumapili February nne mwaka huu 2018.  

Akizungumza na Viongozi wa chama cha mapinduzi CCM Tarafa ya Mlangali ambao ni waandaaji wa Sherehe hizo Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa bw, Bakari Mfaume amewaalika wanachama, wapenzi na wakereketwa wa chama hicho kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili Katika viwanja vya CCM Mlangali ili kushiriki Sherehe hiyo Kubwa ya Miaka 41 Tangu kuzaliwa kwa Chama hicho. 

Aidha katibu wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Ludewa amesema kuwa Katika kusherekea Sikukuu hiyo ya chama cha mapinduzi Uongozi wa chama umeandaa utaratibu wa kuwatembelea Wagonjwa Katika Kituo Cha Afya Mlangali pamoja Na kufanya Usafi katika kituo hicho cha Afya, Kuwatembelea Mabalozi pamoja na Shughuli mbalimbali kwakuwa Chama hicho ni cha wananchi. 

Mgeni Rasmi Katika Sherehe hiyo Atakuwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Bw, Erasto Ngole maarufu kwa jina la Shikamoo Parachichi Lengo ni Kuboresha Uhai wa chama,Kuongeza wanachama Wapya ndani ya chama hicho pamoja na Kuendelea Kuonesha Imani kwa wanachama na wananchi wa wilaya ya Ludewa ili waendelee kuzitambua kazi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya chama cha mapinduzi.

Baadhi ya Viongozi Na wananchi wa kata ya Mlangali Akiwemo Diwani wa Kata hiyo ya Mlangali Mh, Hamis Kayombo wamesema kuwa wamejiandaa vyema Tayari kwakusherekea Sikukuu ya Miaka 41 Tangu kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM chama ambacho kinaongozwa na Mwenyekiti Shujaa Dr. John Pombe Magufuli ambae ni Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Chama cha mapinduzi CCM kinatimiza miaka 41 Tangu kuzaliwa kwake huku ilani yake ikiendelea kutekelezwa kwa ubora Mkubwa na viongozi wa Serikali chini ya Rais Dr. John pombe Magufuli ambapo wananchi wa Tanzania imani yao nikuona kuwa Kero na matatizo yao yanatatuliwa kwa muda muafaka na viongozi waliowekwa Madarakani.

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking