Dinsdag, Februarie 06, 2018

WILAYANI LUDEWA WAMSINDIKIZA KWA MINOFU NA ZAWADI MKUU WA SHULE,,






Na Maiko Luoga Ludewa

Ni katika Hafla ya Kumuaga Mkuu wa Shule ya Sekondari Montfort Brother Joseph John (JJ) Iliyofanyika Jana February 05/2018 katika Ukumbi wa Shule hiyo Iliyopo katika kijiji cha Masimbwe kata ya Lubonde wilayani Ludewa Katika Mkoa wa Njombe na Kumkaribisha Mkuu mpya wa Shule hiyo Brother Masini Ambae Ni Raia wa Hapa Tanzania.

Brother Joseph John Ambae ni Raia wa Kutoka Nchini India Alianzisha shule hiyo tangu mwaka 2007 na kufanya Kazi katika Shule hiyo ya Sekondari St. Montfort Masimbwe inayomilikiwa na Kanisa Catholic yenye makao makuu Roma huko nchini Italy akiwa Kama Mkuu wa Shule na Sasa Mwalimu huyo anaondoka na Kumuachia Kijiti Mtanzania Masini Ili aweze Kuendeleza Taaluma katika Shule hiyo.

Hafla hiyo ya Kumuaga Mwalimu Joseph John na Kumkaribisha Mwalimu Masini Jana Ilihudhuriwa pia na Muhashamu Baba Askofu wa Kanisa Roman Catholic Jimbo la Njombe Alfred Maluma aliyetoa wito kwa mkuu mpya wa Shule ya sekondari Montfot kufuata nyayo za Aliyekuwa Mkuu wa Shule hiyo hasa katika mambo mema ya Kuiendeleza Shule hiyo ikiwemo kukuza Kiwango cha Elimu.

Baadhi ya Walimu, Wanafunzi pamoja na wazazi walioshiriki Kuagwa kwa Mkuu huyo wa Shule Raia wa India walimzungumzia Brother Joseph John Kuwa alikuwa kiongozi wa Kujituma akiwa katika Shule hiyo katika Kutafuta miundombinu ya Kuboresha shule hiyo huku wakisema kuwa wanaamini kuwa Hata mwalimu anayeshika nafasi yake ataendeleza mazuri aliyoyaacha Mwalimu Joseph John.

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking