Vrydag, Maart 02, 2018

Ushuru wa bidhaa za chuma yaleta utata baina ya Trump na Wafanyabiashara

Galvanized coiled steel at the ThyssenKrupp steelworks on January 17, 2018 in Duisburg, Germany
Washirika wakubwa wa biashara wa Marekani wamekasirishwa na tangazo la Rais wa nchi hiyo Donald Trump juu ya mpango wa kutoza ushuru kwa bidhaa za chuma na aluminiam zinazoingizwa.

Umoja wa Ulaya na Canada kwa pamoja zimesema zitafanyia kazi uamuzi huo, kupingana na tamko hilo.
Rais wa Tume ya Ulaya Jean Claude Juncker amesema uamuzi huo wa Marekani wa kutoza ushuru utahatarisha maelfu ya kazi barani Ulaya.
Nchi za Mexico, China na Brazil wanasema wataziangaliz hatua za kulipiza kisasi.
Bw Trump aliweka ujumbe katika akaunti yake ya Twitter na kusema Marekani ilikuwa imekumbwa na "sera mbovu na zisizo sawa za biashara".
Alisema bidhaa za chuma zinazo ingizwa zingetozwa ushuru ya asilimia 25 na aliminiam asilimia 10.
Lakini wakosoaji wake wamesema ushuru hizi hazitafanikiwa kulinda ajira za Marekani na hatinaye zingepandisha bei za bidhaa kwa wanunuzi.
Habari ziliathiri hisa za Asia ambazo zilishuka siku ya Ijumaa, huku hisa ya Japan, Nikkei ikipoteza zaidi ya asilimia 2.
Hisa za kampuni kubwa ya magari ya Japan, Toyota zilishuka na zaidi ya asilimia 2 na hisa za Nippon Steel pia zilishuka kwa zaidi ya asilimia 4.
Toyota imesema maamuzi ya Marekani " yangeathiri sana watengeneza magari na wanunuzi"

A worker at the Tamco steel mini mill in Rancho Cucamonga, California. October 4, 2002

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking