Donderdag, Maart 01, 2018

Vifo na uharibifu mkubwa waripotiwa Ghouta Syria

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeambiwa kuwa vifo, uharibifu mkubwa na taabu vimeendelea kutokea eneo la Ghouta nchini Syria, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

Mkuu wa masuala ya dharura wa umoja wa mataifa Mark Lowcock, amesema vita vinavyoendelea na kuzuiliwa kuingia katika eneo walilopo raia wa kawaida inamaanisha kuwa hakuna msaada utakaoweza kuwafikia.

Ameongeza kuwa kusitishwa mapigano kwa saa tano pekee hakutoshi kuwafikia maelfu ya watu waliomo sehemu hiyo.

Wajumbe wa Marekani wameilaumu serikali ya Syria na washirika wake kwa kushindwa kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda.

Mjumbe wa Urusi amesema waasi wanaoungwa mkono na Marekani na washirika wake ndio wakulaumiwa.


Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking