Saterdag, Februarie 03, 2018

Dancer wa Diamond Awaangushia Kichapo Shilawadu

Watangazaji wa Kipindi maarufu cha Shilawadu kinachorushwa na Clouds tv,Soudy Brown na Kwisa wamechezea kichapo kutoka kwa Dancer wa Diamond,Mose Iyobo,usiku wa kuamkia  ijumaa,baada ya kutaka kumuhoji kuhusu matukio yaliyotokea hivi karibuni kati ya familia yake na mwanadada Tunda.

Wakithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Shilawadu wameandika katika ukurasa wao wa instagram:

Kazi yetu ina changamoto kubwa sana..asilimia kubwa ya ma star wanatuunga mkono.

Usiku wa Leo wakati tukiwa kazini tumenusurika kumwagwa damu na mtu tuliemfuata kumuomba kufanya naye mahojiano,kati yetu kuna walioumia viuno,mikono, etc.kuna uharibifu wa vifaa vyetu vya kazi umetokea pia,wenzetu wanaendelea na matibau Mungu  ni mwema  Mungu ni wetu sote na hili litapita bado tuna wasiwasi tu kama mhusika ataendelea kututafuta kwa ajili ya kutudhuru zaidi,tunasikitishwa sana na matumizi ya nguvu dhidi yetu sisi Wanyonge #Shilawadu

Kuna watu watasema Shilawadu wamezidina kusahau kuwa sisi ni wana Habari kama wanahabari wengine na kupata habari ni haki ya kila mwananchi kama ilivyo haki nyingine yoyote ile.Kifungu cha 18 cha katiba  ya Jamhuri ya Muungano 1977 na hatimaye kufanyiwa marekebisho mwaka 2005 inampa haki mtu na uhuru wa kujieleza na kutoa mawazo,uhuru wa kutafuta habari,kupata habari,na kuneza habari bila kujali mipaka,pia sheria hiyo inampa haki mtu ya kuwasiliana bila kubughudhiwa na mawasiliano na kufahamishwa wakati wowote masuala yoyote muhimu yahusuyo maendeleo yake na yahusuyo jamii yake kwa ujumla

,,,,,,,,,,,,,,,,

Kazi Yetu Ina Changamoto Kubwa Sana.... Asilimia kubwa Ya Ma Star wanatuunga Mkono . Ucku Wa Leo Wakati Tukiwa Kazini Tumenusurika Kumwagwa Damu na Mtu tuliemfata Kumuomba kufanya nae Mahojiano, Kati yetu kuna walio umia Viuno Mikono e.t.c kuna uharibifu wa Vifaa vyetu Vya kazi umetokea Pia, Wenzetu wanaendelea na Matibabu Mungu ni Mwema Mungu Ni Wetu Sote na Hili Nalo Litapita, Bado Tuna Wasiwasi Tu kama Mhusika ataendelea Kututafuta Ucku huu kwa ajili ya Kutudhuru Zaidi, Tunaskitishwa sana na Matumizi makubwa ya nguvu dhidi yetu sisi Wanyonge wa #Shilawadu . Kuna Watu watasema Shilawadu wamezidiiii na kusahau kuwa sisi Ni Wana Habari Kama Wana Habari Wengine . Na Kupata habari ni haki ya kila mwananchi kama ilivyo haki nyingine yoyote ile. Kifungu cha 18 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano 1977 na hatimaye kufanyiwa marekebisho mwaka 2005 inampa haki mtu uhuru wa kujieleza na kutoa mawazo, uhuru wa kutafuta Habari, kupata Habari na kueneza habari bila kujali mipaka. Pia Sheria hiyo Inampa haki pia ya mtu kuwasiliana bila kubughudhiwa na mawasiliano hayo na kufahamishwa wakati wowote masuala yote muhimu yahusuyo maendeleo yake na yahusuyo jamii yake kwa ujumla . Panapo Majaliwa Tukutane Ijumaa Hii kwenye @shilawadu Saa Tatu Kamili Ucku . Imeandikwa Na Mtaarishaji wa Kipindi Cha Shilawadu Benedict Noel

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking