Dinsdag, Februarie 06, 2018

HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA AMESEMA


Polisi nchini Maldives imemkamata Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu nchini humo huku mgogoro wa kisiasa ukiendelea kuwa katika hali mbaya kwenye nchi hiyo iliyoko katika bahari ta Hindi.

Jaji Mkuu Abdulla Saeed na Jaji Ali Hameed, walikamatwa na polisi baada ya nchi hiyo kutangaza hali ya hatari huku kukiwa hakuna maelezo yaliyotolewa na uchunguzi au mabadiliko juu ya mtafaruku huo ulipata kasi baada ya rais wa nchi hiyo Abdulla Yameen alipokataa kutii amri ya Mahakama ya kuwaachilia wafungwa wote wa kisiasa.

Maldives ni taifa dogo katika bahari ya Hindi likiviunganisha visiwa vidogo 1,192 na utalii ndiyo chanzo kikubwa cha mapato ya nchi hiyo. Wiki iliyopita Mahakama ya juu nchini humo iliamuru kuachiwa kwa wanasiasa wa upinzani na pia Mahakama hiyo iliamua kwamba mashitaka ya rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Nasheed ya mwaka 2005 ambaye yuko uhamishoni yalikuwa kinyume na katiba.

Hatua hiyo ya Mahakama ya juu ilifuatiwa na tamko la Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi ambaye alisema kuwa atatekekeleza amri ya Mahakama na mara baada ya kauli hiyo kamishna huyo alifukuzwa kazi na Rais Adulla Yameen huku jeshi la nchi hiyo likiamuriwa kukataa kumuondoa Rais Yameen madarakani.

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking