Maandag, Februarie 05, 2018

Mke wa Majuto: Nilikua nakesha nikimuombea Mume wangu


MKE wa mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athuman ‘Majuto’, Aisha Yusuf amesema kuwa siku za hivi karibuni alipoanza kuugua tena mumewe amekuwa akikesha na kumuombea arudi katika hali ya kawaida kwani anapoumwa vitu vyote vinalala.

Mke huyo alisema mume wake ni mcheshi sana na ni mtu anayeifanya familia kuwa na furaha kila wakati sasa anapokuwa mgonjwa nyumba inakuwa haina amani kabisa na hata watoto ambao amezoea kucheza nao wanapoa.

“Kila siku dua zangu ni kwa mume wangu maana ndiyo nguzo katika familia yetu na ni mtu mcheshi sana kwa familia hivyo namuombea sana apone maana ndiye furaha yangu,“ alisema mke wa Majuto.

Chrispiny kalinga blog

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking